Anne Njeri amwanga mtama

  • | Citizen TV
    13,514 views

    Mfanyabiashara kwenye utata wa shehena ya mafuta ya shilingi bilioni 17 Anne Njeri Njoroge sasa anawataja baadhi ya watu anaosema wanahusika na kuhangaishwa kwake. Mfanyabiashara huyu ameelezea namna alivyokutana na baadhi ya watu hawa akiwemo waziri na hata mbunge mmoja wa Kenya Kwanza. Katika mahojiano ya kipekee na mwanahabari wetu Seth Olale, Ann Njeri ameelezea kwa mapana masaibu yake, huku akielezea kuamrishwa kwake kujisalimisha mara moja katika afisi kuu za idara ya Jinai