- 11,892 viewsDuration: 1:48Mwili wa mshawishi wa mtandaoni, Ashly Robinson, anayefahamika zaidi mtandaoni kama Ashlee Jenae, unatarajiwa kuagwa Jumatatu na Jumanne na kisha kufuatiwa na ibada ya mazishi itakayofanyika katika jimbo la New Jersey, nchini Marekani. Moja ya wanafamilia wa karibu ameiambia BBC kuwa maandalizi ya mazishi yanaendelea na kwamba familia, marafiki na mashabiki wa Ashlee watapata fursa ya kushiriki katika zoezi la kuaga mwili pamoja na ibada ya mazishi. Mwanzoni mwa juma, ripoti za baadhi ya vyombo vya habari zilieleza kuwa mwili wa Ashlee Jenae ulirejeshwa kutoka Tanzania na kukabidhiwa kwa familia yake Ijumaa iliyopita Mwandishi wa BBC @lasteck2024 - - #bbcswahili #ashley #marekani #zanzibar #fyp Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw