Skip to main content
Skip to main content

Askofu Anyolo ataka suluhu ya haraka kukomesha mzozo Mwingi

  • | Citizen TV
    675 views
    Duration: 3:24
    Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Nairobi, Philip Anyolo, ameitaka serikali kutafuta suluhu ya haraka kumaliza mgogoro kati ya jamii mbili huko Mwingi, Kaunti ya Kitui, ili kuzuia maafa zaidi. Anyolo, aliyezungumza huko Wote, Kaunti ya Makueni, pia ameonya wanasiasa dhidi ya kuchochea jamii zilizo katika mpaka wa Tseikuru kuendelea na mapigano na kuvuruga amani. Ombi lake limejiri huku Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen akisema kuwa serikali imedhibiti hali mpakani humo, akiahidi kutoshuhudiwa kwa tukio kama la Jumamosi iliyopita tena.