Askofu Isaiah Deye asema hataki hatamu nyingine

  • | KBC Video
    360 views

    Askofu msimamizi wa kanisa la Methodist humu nchini, Rev. Isaiah Deye sasa amesema atahudumu muhula mmoja pekee. Akihutubia mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa kanisa hilo katika kanisa la Methodist huko Nkubu, Deye alitoa wito wa kukomeshwa kwa mizozo ya uongozi, akionya kwamba hali hiyo inahujumu ufanisi ulioafikiwa kanisani. Aidha alikariri kwamba hatawania kuchaguliwa tena, ambapo aliahidi kuondoka mwishoni mwa hatamu yake ya miaka mitano ili kutoa fursa kwa uongozi mpya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive