Askofu mkuu Anthony Kivuva Musonde wa dayosisi ya kanisa katoliki ya Mombasa ametoa wito kwa wakenya kudumisha upendo, umoja na kutofanya mambo kwa pupa nchi hii inaposherehekea sikukuu ya krismasi. Akizungumza kwneye makazi yake mnamo mkesha wa krismasi Askofu mkuu Kivuva alisema kuwa msimu huu wa sikukuu unafaa kuwa muda wa familia kuungana tena, kuwa wale wasiojiweza na kudhihirisha uwiano wa kitaifa badala ya migawanyiko ya kidini, kikabila na kijamii.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive