Askofu Mkuu Jackson Ole Sapit ataka wanasiasa kulegeza misimamo yao ya kisiasa

  • | Citizen TV
    502 views

    Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Jackson Ole Sapit, amezitaka pande hasimu za kisasa za Kenya Kwanza na Azimio la Umoja kusitisha misimamo mikali huku mazungumzo kati ya viongozi wa makundi hayo yakiandaliwa. Askofu Sapit pia anataka Azimio isitishe vitisho vya kuandaa mandamano na kushiriki mazungumzo kikamilifu baada ya Rais William Ruto na Kinaara wa Azimio kukutana. Aidha viongozi wa kisiasa wameshauriwa kuweka tofauti zao kando na kuliweka taifa mbele kwenye mazungumzo ya uwiano.