Askofu mkuu Philip Anyolo awataka wanasiasa pia wafunge Kwaresma

  • | Citizen TV
    307 views

    Askofu mkuu wa kanisa katoliki dayosisi ya Nairobi Philip Anyolo amewataka viongozi wa kisiasa kujiunga na kanisa katika kipindi cha siku 40 za Kwaresma kutafakari uadilifu wao binafsi. Akizungumza katika kanisa la Mtakatifu Monica eneo la Njiru wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kwaresma, Askofu Anyolo amesema kauli ya mwaka huu ya “uadilifu kwa taifa lenye haki” ina maana kubwa kwa wakenya wakati huu ambapo viongozi wanaonekana kukiuka sura ya sita ya katiba. Askofu anyolo pia ametoa wito kwa serikali kuu kutafuta mbinu za kupunguza gharama ya maisha .