Askofu mkuu wa katoliki jimbo la Nyeri ataka ukaguzi wa utajiri wa wahubiri

  • | Citizen TV
    1,099 views

    Askofu Mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Nyeri Antony Muheria ametaka ukaguzi wa mali ya wahubiri na viongozi wote wa kidini ili kukabiliana na itikadi potofu inayojitokeza nchini. Askofu Muheria akisema wahubiri wengi wamekuwa wakijitafutia utajiri kwa kuhuburi, badala ya kuendeleza mambo ya kidini. Muheria akisema yuko tayari kutangaza mali yake, akisema huu ndio utakuwa mwanzo wa kudhibiti makundi ya kidini yanayochipuka kila uchao. Alikuwa akizungumza kwenye kikao na wanahabari, ambapo ameendeleza shutuma zake dhidi ya yanayoendelea eneo la Shakahola kaunti ya Kilifi