- 830 viewsDuration: 1:45Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Nyeri Anthony Muheria amelalamikia kuwa huduma katika hospitali zinazoendeshwa na madhehebu mbalimbali zinaelekea kukwama kutokana na madeni ya SHA ambayo serikali haijalipa. Muheria ameirai serikali kuwajibika kwani wakenya wengi wataathirika iwapo hospitali hizo zitakosa kutoa huduma.