Askofu Oginde ahimiza wanasiasa kutumia busara kwenye swala la BBI

  • | KBC Video
    Askofu David Oginde wa Kanisa la Christ is the Answer Ministry CITAM, amewahimiza wanasiasa wawe na busara wakati wa majadiliano yanayoendelea kuhusu ripoti ya BBI. Akiongea katika hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo katika Ukumbi wa Bomas, Askofu Oginde amesema mjadala huo haufai kutumiwa na wanasiasa kuwagawanya Wakenya. Amesikitika kwamba taifa hili lina mazoea ya kuweka siasa kila kitu hata masuala yaliyo na umuhimu wa kitaifa na kuwahimiza viongozi wanaotofautiana kuja pamoja kwa ajili ya manufaa ya taifa. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #KBCNewsHour #KBClive