Atembea kutoka Pakistan hadi Mecca kutimiza ndoto ya Hajj

  • | BBC Swahili
    630 views
    Akiwa amebeba mwavuli na begi lake, mwanafunzi wa Pakistan ametembea zaidi ya kilomita 4,000 kufikia ndoto yake ya kufika Mecca kwa miguu kabla ya Hija ya mwaka huu. Akianza safari yake ya miezi sita kutoka mji alikozaliwa wa Okara, Usman Arshad alipitia Pakistan, Iran, Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia na hatimaye kufika mji mtakatifu wa Mecca. #bbcswahili #mecca #iddelhajj