Ati ati kuhusu shule kufunguliwa kesho huku shule zaidi ya 150 zikiwa zimefurika

  • | Citizen TV
    3,596 views

    Huku shule zikitarajiwa kuanza kufunguliwa hapo kesho, kuna wasiwasi kuwa huenda shule 150 zikakosa kufunguliwa kwa muhula wa pili wa masomo. Katika baadhi ya maeneo, shule pia zimeendelea kutumika kama hifadhi ya waathiriwa wa mafuriko nchini. Na kama Gatete Njoroge anavyotuarifu, Viongozi wa makanisa na hata baadhi ya wanasiasa sasa wanataka serikali kuahirisha ufunguzi wa shule kwa usalama wa wanafunzi