Skip to main content
Skip to main content

Atwoli aunga mkono nyongeza ya mishahara iliyotangazwa na Ruto

  • | Citizen TV
    528 views
    Duration: 1:35
    Katibu wa Chama cha Wafanyakazi COTU Francis Atwoli sasa amesema kuwa nyongeza ya mishahara iliyotangazwa hapo jana na Rais William Ruto itawafaidi wafanyakazi wote, wala si wale wa mapato ya chini pekee. Akizungumza Kaunti ya Kisumu hii leo, Atwoli alisema kuwa nyongeza hiyo itaimarisha hadhi ya maisha ya Wakenya, hasa wale ambao hawajapata nyongeza ya mshahara kwa muda. Aidha, alimpongeza Rais kwa hatua hiyo, ambayo alisema inafuata nyayo za marais wa awali. Rais Ruto alitangaza nyongeza ya asilimia 12 ya mapato ya jumla, na asilimia 15 ya mapato ya wafanyakazi katika sekta ya kilimo.