Azimio yawasilisha kesi kupinga sheria tata ya fedha

  • | Citizen TV
    1,513 views

    Muungano wa Azimio la Umoja sasa umewasilisha kesi mahakamani kutaka kujumuishwa kwenye kesi inayopinga utekelezwaji wa sheria mpya ya fedha. Azimio wakitaka kujumuishwa kwenye kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani na Seneta wa Busia Okiya Omtata, na iliyopangiwa kusikilizwa hapo kesho. Haya yakijiri huku bunge la taifa ambalo limeshtakiwa kwenye kesi hiyo vile vile likiwasilisha hoja yake inayotetea sheria hiyo mpya