Baadhi ya makasisi wapinga udhibiti wa makanisa na serikali

  • | Citizen TV
    631 views

    Baadhi ya wahubiri wa dini waliofika mbele ya kamati maalum ya seneti inayochunguza mauaji ya Shakahola imepinga kudhibitiwa kwa makanisa wakisema makanisa yafaa kuwachwa kujisimamia. Akizungumza alipofika mbele ya maseneta, Askofu wa kanisa la Jesus is Alive Ministries Margaret Wanjiru amekashifu kile alichotaja ni kuhangaishwa kwa makanisa baada ya matukio ya Shakahola.