- 4,450 viewsDuration: 1:50Viongozi wa Kenya Kwanza wameshutumu kampeni ya Muungano wa Upinzani katika Kaunti ya Bomet iliyoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Wakizungumza katika Kaunti ya Kericho, viongozi hao wanaoiunga mkono serikali walimtetea Rais William Ruto, wakisema kuwa ukosoaji wa upinzani hauna msingi na haujaambatana na ajenda madhubuti ya maendeleo. Wakiongozwa na Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot na Gavana Erick Mutai,viongozi hao walisema kuwa utawala wa Kenya Kwanza unaendelea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi bila kuyumbishwa na siasa za upinzani. Aidha walikosoa matamshi ya hivi karibuni ya Gachagua kuwa jamii ya Kalenjin haina uongozi thabiti. Viongozi hao walitaja kauli hizo kuwa za kusikitisha na zisizo na ukweli, wakisisitiza kuwa eneo hilo lina viongozi wenye uwezo wa kutetea na kuendeleza maslahi ya wakazi wake.