- 2,844 viewsDuration: 1:11Mbunge wa Saboti Caleb Amisi anasema yeye pamoja na wenzake katika mrengo wa Linda Wananchi hawatahudhuria mkutano wa kitaifa wa wajumbe wa ODM unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 mwezi huu. Amisi amedai kuwa mkutano huo unakiuka katiba ya chama, akisisitiza kuwa ni lazima uitishwe rasmi na Katibu Mkuu Edwin Sifuna kufuatia uamuzi wa mahakama uliomrejesha mamlakani.