Baadhi ya wabunge wa Mlima Kenya walipiga kura kumtimua Gachagua

  • | Citizen TV
    6,272 views

    Kura za Wabunge 282 za kumbandua Naibu Rigathi Gachagua ofisini dhidi ya Wabunge 44 waliolenga kumnusuru imefichua Ukuruba unaoshamiri kati ya Serikali na Upinzani. Aidha, Katika Dhoruba Kali inayomkabili Naibu Rais amekumbana na upinzani mkubwa Katika Ngome yake huku Wabunge wengi wakionekana kujitenga naye. Upigaji Kura ulionekana kushawishiwa Pakubwa na Misimamo ya Chama, huku Chama cha Wiper Kikijitokeza kumtetea Naibu rais bila mafanikio.