Baadhi ya wabunge wa ODM watisha kuelekea kortini

  • | Citizen TV
    1,156 views

    baadhi ya wabunge wa chama cha ODM sasa wametishia kuchukua hatua za kisheria kufuatia azimio la kuwafurusha wanachama watano kwa madai ya kuunga mkono mrengo wa Kenya Kwanza. Akizungumza katika ibada kwenye kanisa la Uriri huko Migori, mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi alisisitiza kuwa alifanya mkutano na Rais Ruto ili kupata miradi ya maendeleo itakayowafaa wakazi wa eneo bunge lake. Aidha, mwenzake wa Uriri Mark Nyamita alitoa kucha kwa usimamizi wa chama cha chungwa akidai kuwa hakukuwa na haki katika kufikia uamzuzi huo.