Skip to main content
Skip to main content

Baadhi ya walimu wa sekondari msingi wapendekeza mabadiliko

  • | Citizen TV
    234 views
    Duration: 1:02
    Baadhi ya walimu wa sekondari msingi kutoka kaunti ya Nandi wametoa wito kwa idara ya elimu nchini kusaidia shule za sekondari msingi kujisimamia ili kutatua changamoto wanazozipitia mara kwa mara. Wakiongozwa na katibu wao Stephen Lagat, walimu hao wanasema kwamba hawataki kuwa chini ya uongozi wa shule za msingi jinsi ilivyo kwa sasa. Kulingana na walimu hao, usimamizi chini ya walimu wakuu wa shule za misingi umekuwa na dosari na kwamba ni tishio kwa masomo ya JSS.