Barabara ya Mwangati Kuresoi Kusini haipitiki msimu wa mvua

  • | Citizen TV
    264 views

    Wakazi wa Wadi ya Tinet katika eneobunge la Kuresoi Kusini wameandamana wakilalamikia hali mbaya ya barabara ya Mwangati hadi Kiwanda cha Chai cha Chemusian. Wakazi hao waliokusanyika Kapkembu, na kutembea umbali wa kilomita kadhaa wanaishinikiza serikali kukarabati barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa usafirishaji wa mazao ya kilimo. Wakazi hao wamelalamika kuwa bali na hasara ya mazao, hali hiyo imeathiri pia huduma za dharura.