Baraza la makanisa nchini lamwandikia Rais Ruto waraka

  • | Citizen TV
    733 views

    Baraza la makanisa nchini NCCK limeilaumu serikali ya kenya kwanza kwa kuongeza ushuru kinyume na ahadi ilizotoa, kutoheshimu sheria, na kukosa kuwasikiliza wananchi. Baraza hilo limemkosoa rais william ruto likisema ushuru wa nyumba za bei nafuu pamoja na makato ya bima ya afya umepunguza mno mapato ya waajiriwa. NCCK limemshauri rais abuni jopo litakaloangazia changamoto za uchumi wa taifa.