Basi lenye abiria lasombwa na maji yenye fujo

  • | BBC Swahili
    2,753 views
    Tazama namna kikosi cha huduma za dharura kilivyowaokoa abiria waliokuwa wamenasa ndani ya basi lililokwama kwenye mafuriko katika barabara kuu yenye shughuli nyingi kaskazini mwa Kenya. Basi hilo, lililokuwa na takriban abiria 50, lilikuwa likielekea mji mkuu, Nairobi, likitokea kaunti ya Wajir. Dereva alijaribu kuvuka sehemu ya barabara iliyofurika maji na basi hilo likakwama kwenye tope ndipo lilipozingirwa na maji yenye kasi. Baadhi walipanda juu ya basi na waliokuwa ndani ya basi hilo walifanikiwa kutoka kupitia madirishani. Katika wiki iliyopita, taifa hilo la Afrika Mashariki limeshuhudia mvua kubwa zinazotabiriwa kuendelea. #bbcswahili #kenya #mafuriko Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw