Benard Membe : 'Nitagombea urais upinzani ukinipa ridhaa'

  • | BBC Swahili
    Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe, anasema ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu. Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchini matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli. #Tanzania #Uchaguzi #Siasa #bbcswahili