BIDEN ATIA SAINI AMRI ZA KIUTENDAJI KUHUSU JANGA LA COVID-19

  • | VOA Swahili
    Rais wa Marekani, Joe Biden ametumia siku nzima ya jana Alhamisi kutia saini amri kadhaa za kiutendaji kushughulikia jinsi ya kukabiliana na janga la virusi vya corona, ambalo limewaathiri zaidi watu hapa nchini Marekani kuliko sehemu nyingine yoyote duniani. Marekani ina zaidi ya kesi milioni 24 Covid 19 kati ya kesi milioni 97 kote ulimwenguni.