Miaka ya nyuma si wanawake wengi waliojitosa katika biashara za kuajiriwa lakini wachache waliojitolea walionekana kufanya kazi kwa dhati. Wanapotajwa, jina la assumpta ndave raphael haliwezi kukosekana kwani licha ya pandashuka alizopitia kujitafutia riziki na kuwalea wanawe, sasa amekuwa jina la kutajika katika sekta ya mawasiliano, huku akiwa miongoni mwa wafanyibiashara wanaoenziwa na kampuni ya safaricom tangu ilipoanza kutoa huduma zake humu nchini. Kwa upande wake assumpta sasa anajivunia kuwa mwajiri na mfanyibiashara mahiri huku wanaomfahamu wakimtaja kama mwanamke mwenye bidii ya hali ya juu. Ni kutokana na hayo ambapo hii leo ndiye tunayemvisha taji la mwanamke bomba