Binamuye mtoto Junior Sagini kufungwa miaka 40 jela

  • | Citizen TV
    2,087 views

    Mahakama kuu mjini Kisii imemfunga miaka 40 gerezani mshukiwa mkuu kwenye kesi ya kung'olewa macho kwa mtoto Junior Sagini mwaka jana. Maina Ochogo ambaye ni mpwa WA mtoto huyu amehukumiwa pamoja na Pacificah Nyakerario aliyefungwa miaka 10 naye Nyanyake Sagini Rael Nyakerario akipewa hukumu ya miaka 5 gerezani. watatu hawa sasa wana siku 14 kukata rufaa