- 142 viewsDuration: 1:32Bodi ya kusimamia maji mjini wote kaunti ya Makueni WOWASCO imeanzisha msako wa kukabiliana na waliojiunganishia maji na ambao wamekuwa wakikwepa kulipa kodi ya maji mjini wote. Afisa mkuu wa bodi hiyo Albanus Ndunda anasema wamegundua kuwa asilimia 32 ya maji yamekuwa yakipotea mikononi mwa wezi wa maji hali ambayo imewafanya wakazi wa mji huo kukosa maji mara kwa mara.