Brigedia Swaleh Said Nzaro azikwa leo alasiri katika eneo la Kikambala kaunti ya Kilifi

  • | K24 Video
    263 views

    Brigedia Swaleh Said Nzaro aliyefariki katika ajali ya jana ya ndege amezikwa leo alasiri katika eneo la Kikambala kaunti ya Kilifi. Wakiongozwa na waziri wa jinsia na utamaduni Aisha Jumwa, viongozi mbalimbali, maafisa wa jeshi wanaohudumu na waliostaafu, jamaa na marafiki wamemuenzi Swaleh kwa kujitolea kwake kudumisha usalama. Alipewa heshima ya mwisho kwa kufyatuliwa kwa mizinga kulingana na desturi ya jeshi. Kwengineko familia mbili kaunti ya Kirinyaga zinaomboleza kifo cha Sajini mwandamizi john Kinyua Muriithi kutoka kijiji cha Kirimunge na Sajini Rose Nyawira kutoka eneo la Kagio huko Mwea.