- 5,938 viewsDuration: 2:52Miezi tisa baada ya afisa mmoja wa polisi kujeruhiwa na kupokonywa bunduki aina ya AK-47 huko Mavoko, Kaunti ya Machakos, bunduki hiyo imepatikana mikononi mwa mshukiwa wa ujambazi aliyeuawa katika makabiliano ya risasi na polisi huko Matungulu, Machakos. Mshukiwa huyo aliuawa huku mwenzake akitoroka akiwa na majeraha ya risasi. Kama anavyoarifu Odee Francis, wapelelezi sasa wanachunguza jinsi silaha hiyo ilivyotumika, kwani ilikuwa na risasi 11 pekee ilhali iliibwa ikiwa na risasi 30.