Bunge la Tanzania latetea hatua ya Rais Suluhu

  • | Citizen TV
    6,319 views

    Wabunge wa Tanzania wamemuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuhusiana na hatua zilizochukuliwa za kuwakamata na kuwafukuza wanaharakati wa Kenya waliosafiri nchini humo kuhudhuria kesi dhidi ya mwanasiasa Tundu Lissu. Kwenye mjadala wa bunge la Tanzania, wabunge hao wamemtaka rais samia kuwadhibiti wanaojaribu kuingilia masuala ya nchi hiyo na kutatiza amani. Aidha wamepinga dhana kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania ni ukandamizaji na udhalimu.