Bunge laidhinisha kupelekwa kwa maafisa wa polisi 1000 nchini Haiti

  • | K24 Video
    53 views

    Bunge leo limeidhinisha kupelekwa kwa maafisa wa polisi 1000 nchini Haiti kwa ajili ya kurejesha amani na hali ya utulivu kwa kupambana na makundi ya wahalifu katika nchi hiyo. Wabunge wamekubaliana na ripoti ya kamati maalum ambayo ilipendekeza bunge liidhinishe uamuzi huo. Hata hivyo, hatua ya kuwapeleka itasubiri uamuzi wa kesi iliyowasilishwa mahakamani na kiongozi wa thirdway alliance Ekuru Aokot, kwa sasa, kuna amri ya mahakama ambayo imesimamisha kwa muda polisi kupelekwa haiti hadi kesi iliyo mbele ya Jaji Chacha Mwita itakapoamuliwa.