Buriani Benjamin Mkapa

  • | BBC Swahili
    Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa amezikwa leo katika kijiji cha Lupaso, kusini mwa Tanzania. Baadhi ya Watanzania wanaamini kuwa rais Mkapa atakumbukwa kama muasisi wa Tanzania mpya kwa sababu ya kuanzisha taasisi nyingi katika taifa hilo wakati wa utawala wake kuanzia mamlaka ya kukusanya kodi mpaka taasisi ya kupambana na rushwa. Bwana Mkapa alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa kutokana na mshtuko wa moyo, familia yake ilieleza. #tanzania #bbcswahili #mkapa #benjaminmkapa