Skip to main content
Skip to main content

Buriani na majonzi Webuye katika ibada ya wafu ya watu 14 waliofariki kwenye ajali Webuye

  • | Citizen TV
    234 views
    Duration: 1:44
    Huzuni ilitanda katika uwanja wa Masinde Muliro Webuye wakati wa ibada ya wafu ya watu Kumi na Wanne walioga dunia kwenye ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Malaha. Ajali hiyo iliyotokea siku ya Jumatatu wiki jana kwenye barabara ya Webuye kulekea Kitale ilihusisha trela ambayo iliwagonga watu waliokuwa wakishuhudia ajali nyingine ya awali iliyohusisha pikipiki. Miongoni mwa walioaga dunia ni watu sita wa familia moja. Jamaa za waathiriwa wakielezea huzuni ya kuwapoteza wapendwa wao katika ajali hiyo. Viongozi katika eneo hilo wakitaka wabunge kuangalia upya sheria ya kudhibiti uendeshaji magari nchini ili kukabiliana na visa vya ajali vinavyokithiri...