- 1,080 viewsDuration: 1:09Shirikisho la soka barani afrika (CAF) limeipokonya Senegal ubingwa wa kombe la mataifa ya Afrika – AFCON ambao walishinda Januari na kuitangaza Morocco kuwa bingwa wa makala ya 35 ya mwaka 2025. Kwa mujibu wa taarifa ya bodi ya rufaa ya CAF, uamuzi ulitokana na ukiukaji wa kanuni za mashindano, hasa vifungu vya 82 na 84 vya sheria za mchuano wa mataifa bingwa Afrika. Kifungu cha 82 kinahusu matokeo ya mechi yanapobatilishwa iwapo timu itabainika kukiuka kanuni muhimu za mashindano huku kifungu cha 84 kikihusu athari za nidhamu au ukiukaji wa sheria, ikiwemo mamlaka ya bodi ya rufaa kurekebisha au kubatilisha maamuzi ya awali iwapo kuna rufaa halali na ushahidi mpya. Tayari shirikisho la soka la Senegal limeeleza kuwa litachukua hatua za kisheria na linafikiria kuwasilisha kesi yao katika mahakama ya mizozo ya michezo ulimwenguni baada ya bodi ya rufaa kuwavua ubingwa huo wa AFCON.