CCTV: Polisi walikawia kumpeleka Ojwang' hospitalini

  • | Citizen TV
    30,771 views

    Runinga ya Citizen imepata picha za kipekee zinazoonyesha namna maafisa wa polisi waliomfikisha marehemu Albert Ojwang' katika hospitali ya Mbagathi hawakuwa na haraka licha ya madai ya polisi kuwa aliondoka kituo cha Central akiwa na majeraha yaliyohitaji huduma za dharura. Kanda hiyo imedhibitisha polisi walichukua zaidi ya dakika 20 kumpeleka katika chumba cha dharura ambako wauguzi walidhibitisha tayari alikuwa amefariki kabla ya kufikishwa hospitalini.