'Chama cha Mapinduzi kitakabiliana na upinzani daraja la nne'

  • | BBC Swahili
    10,788 views
    Chama cha upinzani nchini Tanzania ACT Wazalendo kimefungua kesi katika mahakama kuu nchini humo kupinga hatua ya mgombea wake wa Urais Luhaga Mpina kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Katika uamuzi uliotolewa Agosti 26, 2025 Msajili alibainisha kuwa Mpina hakutimiza vigezo vya uanachama kwa mujibu wa kanuni za chama, akisema kuwa alijiunga ACT-Wazalendo nje ya muda uliopangwa na hivyo hakustahili kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho. Je hatua hii ina maana gani? Martha Saaranga amezungumza na Mwanasheria Edson Kilatu na Charles William mchambuzi wa siasa ambaye anaanza kwa kueleza hatua hii ina maana gani kisiasa? #bbcswahili #tanzania #uchaguzi2025 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw