Chama cha UDM chasema ukosefu wa maafisa wa IEBC ni hatari kwa taifa

  • | Citizen TV
    1,030 views

    Ukosefu wa maafisa wa IEBC nchini ni jambo hatari kwa taifa. Ni onyo la chama cha United Democratic Movement (UDM) ambacho kinasema hali hiyo inahujumu haki za wanachi. Akizungumza kwenye hafla iliyoleta pamoja baraza kuu la chama hicho, kinara wa UDM ambaye pia ni Seneta wa Mandera Ali Roba amesema kuwa wapiga kura katika eneo bunge la Banissa hawajapata mwakilishi bungeni tangu mbunge wao kufariki mwaka jana. Aidha baadhi ya wadi nchini zimekumbwa na hali sawia kutokana na kuwa muundo wa IEBC hauko kamili. Roba sasa anamtaka rais william ruto kufanya hima na kuteua makamishna wapya wa iebc kulingana na agizo la mahakama kuu.