Chama cha Wafanyakazi wa Miwa na Viwanda , kimesitisha mgomo wa wafanyakazi wa viwanda vinne vya sukari vilivyokuwa vya serikali na ambavyo Kwa sasa vimekodishwa.
Katibu wa chama hicho, Francis Wangara, pamoja na mwenyekiti Benard Wanyonyi, wamesema uamuzi huo umetokana na mazungumzo na viongozi wa COTU waliowataka kutoa nafasi kwa mazungumzo na shinikizo kwa serikali kulipa madeni ya shilingi bilioni 20 wanazodaiwa wafanyakazi. Aidha, viongozi hao wamesema iwapo jitihada za COTU hazitazaa matunda, watatangaza hatua kali zaidi ili kufanikisha mchakato huo.