Chama cha walimu chatia saini mkataba na TSC

  • | Citizen TV
    530 views

    Katibu mkuu wa Muungano wa Walimu wa Wanafunzi wenye mahitaji maalum James Torome ametangaza makubaliano na tume ya kuajiri walimu Nchini ambapo zaidi ya 6,000 watahamishwa kutoka shule za kawaida na kujiunga na shule maalum chini ya mpangilio wa awamu tatu. Akizungumza mjini Narok Torome alisema mpango huo utatekelezwa katika awamu tatu huku ya kwanza ikishuhudia kuhamishwa kwa walimu 1,760 ifikapo mwezi Mei mwaka huu. Katika awamu ya pili walimu 2,000 watahamishwa mwezi wa Desemba,huku awamu ya tatu ikihusisha uhamisho wa walimu 2,200 mnamo mwezi Julai mwaka ujao.