Chama cha walimu KUPPET katika kaunti ya Busia wapinga mswada wa fedha

  • | Citizen TV
    152 views

    Viongozi wa chama cha kutetea masilahi ya walimu wa shule za upili na vyuo vya mafunzo KUPPET wameendelea kuelezea upinzani wao kwa mswada wa fedha wa mwaka wa 2023. Wa punde kuelezea upinzani wao ni waalimu kutoka tawi la Busia wanaopinga mswada huo wakikosoa zaidi ada ya nyumba inayolenga kuwakata asilimia tatu ya mishahara yao. Wakiongozwa na katibu mkuu Moffat okisai na mwenyekiti Charles Mukhwana, walimu hawa walishikilia kuwa mpango huu si wa muhimu kwao kwa sasa wakitaka serikali kusitisha mipango yake na mswada huo.