Chama cha Wiper chatishia kuanzisha mchakato wa kumwondoa mamlakani rais Ruto

  • | K24 Video
    85 views

    Chama cha Wiper sasa kinatishia kuanzisha mchakato wa kumwondoa mamlakani rais Willliam Ruto, endapo ripoti ya mazungumzo ya taifa haitaangazia swala la garama ya juu ya maisha. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, viongozi wa chama hicho wakiwemo wabunge pia wameongeza kwamba hawatasita kuwaongoza wakenya katika awamu nyingine ya maandamano ya kitaifa endapo juhudi hizo hazitaangazia maslahi yao.