Changamoto tele katika kuelewa mtaala wa CBE

  • | Citizen TV
    44 views

    Maafisa wa wizara ya elimu eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia wamewahakikishia wazazi na wadau kuwa mikakati kabambe imewekwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta hiyo zikiwemo uhaba wa walimu na miundo msingi duni. Naibu mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Busia Oliver Adika amekiri kuwepo na changamoto zinazokumba sekta ya elimu hasa wakati huu wa mtalaa mpya wa cbe japo serikali ya kitaifa inafanya kila iwezalo kutafuta suluhu ya kudumu.