Changamoto za watu wenye ualbino Burundi

  • | BBC Swahili
    258 views
    "Nilipozaliwa, mama yangu aliniambia kuwa watu walimueleza anipake mkaa, na wengine wakamshauri anitumbukize ndani ya chungu ili ngozi ibadilike iwe nyeusi'' Kuna zaidi ya watu 900 wanaoishi na ualbino nchini Burundi, wengi wao wanapatikana Bujumbura, Gitega na Ruyigi. Wanakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hutofautiana kulingana na eneo wanaloishi. Mwandishi wa BBC @uwasedg Dina gahamanyi amezungumza na mmoja wa watu wenye ualbino na kuandaa taarifa hii #bbcswahili #burundi #ualbino