Chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV)

  • | K24 Video
    41 views

    Chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) ilipoanzishwa nchini mwaka 2019, ilitoa fursa ya kupiga vita pigo la mauti kwa saratani ya mlango wa kizazi, ambayo ni saratani ya pili inayosababisha vifo vinavyotokana na saratani miongoni mwa wanawake baada ya saratani ya matiti. Kufikia sasa, virusi vya saratani ya mlango wa kizazi vinachangia kwa asilimia 99.7 ya visa vyote vya saratani ya mlango wa kizazi, hivyo basi ipo haja ya kutoa hamasa kuhusu chanjo ya hpv kwa wasichana walio kati ya miaka 10 - 15.