Chanjo Yasaidia Kukabili Surua, Rubella na Homa ya Matumbo

  • | K24 Video
    8 views

    Licha ya chanjo kuwepo, magonjwa ya surua, rubella na homa ya matumbo yanaendelea kuhatarisha maisha ya watoto. Katika siku kumi zilizopita, wahudumu wa afya wameendesha kampeni ya kitaifa ya chanjo ambayo inakamilika leo. Mwanahabari Robi Omondi alizuru Hospitali ya Mutuini jijini Nairobi, ambako awali kulikuwa na upinzani kutoka kwa wazazi, lakini baadaye walikubali chanjo. Wakati wa kampeni hiyo, visa vipya vya surua vilibainika na wahudumu wa afya.