Chile: Maelfu ya nyumba zaangamia, mioto zaidi ya 90 inaendelea kuwaka
Mioto ya misituni inayoenea kote katikati mwa Chile imeuwa idadi kubwa ya watu na mamia hawajulikani walipo katika kile kilichokuwa ni janga baya sana la kitaifa nchini humo ambalo halijatokea kwa zaidi ya muongo mmoja.
Mioto hiyo ya misituni ilianza siku kadhaa zilizopita inatishia usalama katika maeneo ya mpaka wa Vina del Mar na Valparaiso.
Miji miwili ya pwani ambayo ni maarufu kwa watalii na ikichanganywa na wakazi zaidi ya milioni moja.
Kanda ya video iliyochukuliwa kwa Droni na Reuters huko eneo la Vina del Mar ilionyesha eneo lote jirani limeungua.
Pedro Quezada alikabiliwa na moto na kuipoteza nyumba yake.
“Upepo ulikuwa mbaya, na joto lilikuwa linaunguza. Hapakuwa na kupumua. Watu walitawanyika kila mahali.”
Mamlaka nchini Chile wameanzisha amri ya kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku katika eneo lililoathiriwa vibaya sana na kupeleka majeshi kuwasaidia zima moto kuzuia kuenea kwa mioto hiyo.
Maafisa wanasema kiasi cha maelfu ya nyumba zimeangamia, huku mioto zaidi ya 90 ikiendelea kuwaka kute Chile.
Sergio na Maria walirejea katika kile kilichokuwa kimesalia kwenye nyumba yao Jumapili kuokoa kile walichoweza kukipata.
Pamoja na vitu venye thamani vya familia, Karakana ya Sergio ilikuwa pia imeungua.
Familia hiyo, hivi sasa wakiwa na miaka 60, wana wasiwasi kwamba itawalazimu kuanza maisha upya.
“Mikono yetu imefungika. Hii ni karakana yangu, tunaishi hapa. Yote tuliyofanya na kukusanya , katika maisha yetu yote.”
Rais Gabriel Boric Jumapili alitangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa na kusema nchi ijiandae kwa habari mbaya zaidi.
Pia alitoa taarifa ya hali ya hivi sasa katika juhudi za kupambana na mioto.
“Tumesema hilo, na tunarejea kusema – leo kipaumbele ni kuokoa maisha kwani bado kuna mioto inayoendelea kuwaka; kuwasaidia majeruhi, na kuidhibiti mioto inayowaka ambayo inaendelea kuzimwa.”
Licha ya kuwa mioto ya misituni siyo ya kawaida wakati wa kipindi cha joto Chile, mlolongo wa mioto hii ya karibuni imekuwa yenye uangamivu zaidi kuliko kawaida – janga baya zaidi tangu tetemeko la mwaka 2010 kutokea ambapo watu takriban 500 walifariki.
#mioto #chile #misitu #maangamizi #nyumba #zimamoto #curfew #polisi
#voa #voaswahili
12 Aug 2025
- The government will also cover the medical expenses of all survivors.
12 Aug 2025
- The nominees will join several committees.
12 Aug 2025
- The Speaker has been on the detectives' radar.
12 Aug 2025
- Interior Cabinet Secretary Kipchumba Murkomen now says no public servant should openly oppose the government of the day, warning that such conduct is both illegal and unconstitutional.
12 Aug 2025
- DAP-K leader Eugene Wamalwa now says there is a plan by President William Ruto to infiltrate the political outfit through frivolous petitions seeking a change in leadership.
12 Aug 2025
- Long-delayed road projects in northern Kenya are set to resume after years of inactivity, Deputy President Kithure Kindiki has said, citing a new funding approach that has brought contractors back to site.
12 Aug 2025
- A woman has been arrested in Bondeni, Nakuru County for allegedly supplying cannabis and cannabis-laced cookies to minors in what authorities describe as a deliberate attempt to lure children into drug abuse.
12 Aug 2025
- The National Police Service Commission (NPSC) is facing mounting internal tensions that threaten to derail the planned recruitment of 10,000 new police officers this September.
12 Aug 2025
- The government will also cover the medical expenses of all survivors.
12 Aug 2025
- The nominees will join several committees.
12 Aug 2025
- "Your energy has carried us this far, and we are loving every moment of it," Harambee Stars told Kenyans
12 Aug 2025
- The DP said the decision by President William Ruto remains in force and is meant to do away with past discriminatory tendencies targeting some communities.
12 Aug 2025
- The Speaker has been on the detectives' radar.