"Chimbuko la hiki kikundi ni mwanangu alikuwa anapokea Kipaimara"

  • | BBC Swahili
    209 views
    Nchini Tanzania kundi la Watoto lijulikanalo kama @tegeta_kids limejizolea umaarufu mkubwa na kujipatia wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii ambapo watoto wa umri kati ya miaka 5 hadi 15 huonesha uwezo wao wa kucheza nyimbo za mahadhi mbali mbali. Mwanzilishi ambaye ni mama muuza maziwa anasema lengo lake ni kufikisha kikundi hiki katika majukwaa ya kimataifa. Mwandishi wa BBC Veronica Mapunda alikitembelea kikundi hiki kilichopo jijini Dar es Salaama na kuandaa taarifa hii. #bbcswahili #tanzania #tegetakids