Christine Kendi anafanya kazi za ufundi Diani na ndiye anayepamba makala ya mwanamke bomba

  • | Citizen TV
    270 views

    Kazi za ufundi Kwa kiwango kikubwa zimeachiwa wanaume.Hata hivyo Christine Kendi amedhihirisha umahiri wake katika kazi za ufundi kiasi cha kuajiriwa kwenye hoteli moja eneo la Diani. Bidii na juhudi zake zimemfanya akapewa nafasi ya meneja wa kiufundi katika hoteli ya Diani Sea Lodge ambako alianza kazi kama fundi wa mabomba na mifereji. Na si hayo tu Christine kendi ndiye mwanamke wa kwanza na wa pekee kuongoza kitengo cha ufundi katika Sekta nzima ya hoteli huko pwani.