Chuma kilichoanguka kutoka angani Kenya si tishio kwwa raia.

  • | BBC Swahili
    1,938 views
    Chuma chenye uzito wa takriban kilo 500 na kipenyo cha mita 2, kilianguka katika Kijiji cha Mukuku katika Kaunti ya Makueni, Kenya, Desemba 30, 2024.⁣ Uchunguzi wa awali wa Shirika la Anga za Juu la Kenya (KSA) imewahakikishia umma kwamba kifaa hiko si tishio la usalama wa raia. Tukio hili linaangazia juu ya kuongezeka kwa shughuli za anga za juu duniani na hatari za uchafu wa angani, kwani vitu vingi vilivyotengenezwa na binadamu katika mzunguko wa dunia vinaweza kusababisha matukio kama hayo.⁣ #bbcswahili #kenya #angazajuu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw